UN Yaikalia Kooni Tanzania Kwa Kuficha Ripoti Ya Ghasia Za Uchaguzi
Kwa mujibu wa wataalamu hao, ghasia zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi huo zilihusisha matumizi ya nguvu kupita kiasi na silaha za moto na maafisa wa usalama, kukamatwa kiholela kwa raia, watu kutoweshwa kwa lazima pamoja na madai ya watu kuteswa.
Aidha, wanadai kuwa kulikuwa na kukatizwa kwa huduma za intaneti na vitisho dhidi ya wanahabari na watetezi wa haki za kibinadamu waliokuwa wakifuatilia matukio hayo.
Tume ya kwanza ya Uchunguzi iliyoanzishwa Novemba 2025 iliwasilisha ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan Aprili 2026, lakini serikali imechapisha muhtasari pekee badala ya ripoti nzima.
Wataalamu wa UN wanasema muhtasari huo haukutaja watu waliohusika na ghasia hizo, haukupendekeza kesi zozote kupelekwa mahakamani wala kubainisha hatua za kuwawajibisha waliohusika.
Aidha, wameibua wasiwasi kuhusu mamia ya watu wanaoendelea kuzuiliwa kwa muda mrefu bila kesi zao kusikilizwa, wakikabiliwa na mashtaka ya uhaini na makosa yanayohusiana na ugaidi.
Wataalamu hao pia wametaja ripoti za kuwepo kwa makaburi ya halaiki, watu wanaoendelea kutoweka na miili ya baadhi ya waathiriwa kuondolewa katika vyumba vya kuhifadhi maiti.
Katika hatua nyingine, wamelaani vitisho na ufuatiliaji dhidi ya mashirika ya kiraia, wanahabari, watetezi wa haki za kibinadamu na mawakili wanaochunguza ukiukaji wa haki za binadamu.
Wametaka uchunguzi huru, wa haraka na usioegemea upande wowote kufanywa ili kuhakikisha waathiriwa wanapata ukweli, haki na fidia.
Pia wameitaka serikali kuchapisha ripoti kamili bila kuchelewa zaidi, huku wakisema wamewasilisha rasmi wasiwasi wao kwa mamlaka za Tanzania.