"Nipo Nipo Sana" -Presha Ya Matokeo Haimtishi Carrick

Kocha wa Manchester United, Michael Carrick, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kujiuzulu nafasi yake ndani ya klabu hiyo licha ya kukabiliwa na changamoto ya matokeo yasiyoridhisha katika michezo ya hivi karibuni.

Carrick amesema bado ana imani na uwezo wa kikosi chake kurejea katika kiwango bora, akisisitiza kuwa kuondoka Manchester United si jambo lililo katika mipango yake kwa sasa.

Kocha huyo amekiri kuwa matokeo ambayo timu imekuwa ikiyapata hayajakidhi matarajio ya mashabiki na uongozi wa klabu hiyo, lakini amedai kuwa suluhisho si kukimbia majukumu bali kufanya kazi kwa bidii ili kurejesha ushindani ndani ya kikosi hicho.

Akizungumzia mustakabali wake, Carrick amesisitiza kuwa amejipanga kuendelea na kazi yake, kubaini maeneo ambayo timu imekuwa ikifanya makosa na kuyafanyia marekebisho ili kuhakikisha Manchester United inaanza kurejea kwenye njia ya ushindi.

Amesema licha ya kukiri kuwa timu haijashinda idadi ya kutosha ya michezo katika kipindi cha hivi karibuni, bado anaamini kuwa kuna nafasi ya kubadilisha mwenendo huo kupitia juhudi za pamoja za wachezaji na benchi la ufundi.

"Kuondoka kwenye kazi hii si jambo litakalotokea. Hatujashinda mechi za kutosha, lakini ninatarajia kuendelea kufanya kazi, kurekebisha mapungufu na kushinda mechi," amesema Carrick.

Kauli hiyo inaashiria dhamira yake ya kupambana na changamoto zinazoikabili klabu hiyo badala ya kukata tamaa wakati ambapo presha ya kupata matokeo mazuri inaendelea kuongezeka.

Manchester United ni miongoni mwa klabu zenye historia kubwa katika soka la England na matarajio ya mashabiki wake huwa makubwa kila msimu, hali inayofanya matokeo mabaya kuwa chanzo cha presha kwa benchi la ufundi na wachezaji.

Kwa sasa, macho ya mashabiki wa Mashetani Wekundu yataelekezwa katika michezo ijayo, wakisubiri kuona iwapo Carrick ataweza kutekeleza ahadi yake ya kurekebisha mapungufu na kuiongoza timu kurejea katika ushindi.

"Kwa sasa kuna matumaini baada ya kuandaa hadi benchi la ufundi.Kuondoka kwenye kazi hii si jambo litakalotokea. Hatujashinda mechi za kutosha, lakini ninatarajia kuendelea kufanya kazi, kurekebisha mapungufu na kushinda mechi," amesema Carrick.