Charlene Na Yunge Endeleeni Na Ndoa,Usalma Umetosha-Polisi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeimarisha ulinzi na usalama kuelekea na wakati wote wa sherehe ya harusi ya Ndugu Isaya Yunge na Charlene Ruto, inayotarajiwa kufanyika leo Novemba 6, 2026, katika Hoteli ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.

​Akitoa taarifa kwa umma kupitia Waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, (DCP) Wilbrod Mutafungwa, ameeleza kuwa shughuli hiyo itakayohudhuriwa na Viongozi wa Kitaifa, Kimataifa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, imewekewa mifumo thabiti ya kiusalama ili kuhakikisha inafanyika katika hali ya amani, utulivu na usalama.

​Kamanda Mutafungwa amebainisha kuwa Jeshi la Polisi limeimarisha doria katika maeneo yote ya nchi kavu, hoteli zitakazotumiwa na wageni, pamoja na kuimarisha doria za boti katika Ziwa Victoria na maeneo mengine yote ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.

​Aidha, amefafanua kuwa kutakuwa na matumizi makubwa ya barabara kuanzia leo na kesho, hususan Barabara ya Makongoro, barabara inayotoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwanza kuelekea katikati ya jiji, pamoja na njia za kuelekea Malaika Beach Resort, uwanja wa ndege na Barabara ya Nyerere kuelekea Kisesa.

​Kufuatia wingi wa wageni watakaohudhuria, Kamanda Mutafungwa amewasihi watumiaji wote wa barabara na wakazi wa Mwanza kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani, huku wakisikiliza kwa umakini maelekezo ya askari wa usalama barabarani ili kuepusha msongamano na kuhakikisha safari za haraka na salama.

​Aidha, Jeshi la Polisi limewakumbusha wananchi kuendelea kudumisha utamaduni wa amani na usalama, na kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za mapema endapo watabaini viashiria vyovyote au watu wenye nia ovu inayoweza kuhatarisha usalama.

Sherehe hiyo inafanyika miezi kadhaa baadsma ya wawili hao kufanya karamu ya utianaji wa pete,hafla ilofanyika Kenya eneo la Kilgori na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo bilionea wa Zimbabwe,marehem Chivayo na wengine wengi.

Charlene ameolewa Tanzania huku dada yake akiolewa nchini Nigeria miaka kadhaa iliyopita.Hakuna ratiba zaidi iliyotolewa kuhusiana na harusi hiyo ya leo.