Jihan Dimachk Atambulishwa Bungeni Tanzania Baada ya Kutwaa Taji
Mrembo wa Tanzania, Jihan Mohin Dimachk, amepokelewa kwa shangwe na nderemo baada ya kutambulishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, Jumatano, Oktoba 28, 2026, kufuatia kutwaa taji la Miss Grand International 2026.
Utambulisho huo uliibua furaha miongoni mwa wabunge, ambao walimshangilia Dimachk kufuatia ushindi wake katika mashindano ya kimataifa yaliyofanyika jijini Bangkok, Thailand, Oktoba 10, 2026.
Dimachk aliwashinda washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani na kuandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kutwaa taji hilo tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 2013.
Safari ya Dimachk katika mashindano ya urembo ilianza miaka kadhaa iliyopita.
Mwaka 2014, alishiriki mashindano ya Miss Tanzania na kumaliza katika nafasi ya pili ya mshindi wa pili, kabla ya kutwaa taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2016.
Mafanikio hayo yalimwezesha kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Universe yaliyofanyika Ufilipino Januari 2017. Baada ya miaka kadhaa akiendeleza shughuli zake za uanamitindo, alirejea katika mashindano ya urembo mwaka huu na kutwaa taji la Miss Grand Tanzania mnamo Agosti 8, 2026.
Katika mashindano ya mwaka huu, Dimachk alikabiliana na washiriki kutoka mataifa mbalimbali, akiwemo Shyare Andrade wa Ecuador, Beau Megan Goos wa Uholanzi na Emoura Pham wa Vietnam.
Katika kipindi cha maswali na majibu, Dimachk alisisitiza umuhimu wa upendo katika kuleta usawa na kuwaunganisha watu bila kujali tofauti zao za dini au mahali wanapotoka.
Taji la mwaka huu ni la 14 tangu kuanzishwa kwa Miss Grand International.
Washindi waliomtangulia ni pamoja na Janelee Chaparro wa Puerto Rico mwaka 2013, Daryanne Lees wa Cuba mwaka 2014, Ariska Putri Pertiwi wa Indonesia mwaka 2016, Luciana Fuster wa Peru mwaka 2023 na Emma Tiglao wa Ufilipino mwaka 2025.
Ushindi wa Dimachk umefungua ukurasa mpya kwa Tanzania na Afrika katika mashindano hayo, huku utambulisho wake Bungeni ukiwa sehemu ya kutambua mafanikio yake katika jukwaa la kimataifa.
Hata hivyo baada ya ushindi huo,watu walianza kufuatilia asili yake









