Familia Tisa Zilizopoteza Maisha Katika Ajali Ya Ndege Florida Zi
Zatambuliwa
Watu tisa waliofariki katika ajali ya ndege binafsi karibu na Greenacres, Florida, Marekani, Novemba 1, 2026, wametambuliwa huku familia zao zikiendelea kuomboleza vifo vya wapendwa wao.
Miongoni mwa waliofariki ni mjasiriamali wa teknolojia Adam Robinson, mwenye umri wa miaka 45, mkewe Helen Sharp, 40, pamoja na watoto wao wawili Emma, miaka minne, na Charlie, miaka miwili.
Waathiriwa wengine ni Rachael Reed, Charmi Fehr, Anita Maria Cetina na marubani wawili waliokuwa wakiongoza ndege hiyo wakati wa ajali.
Katika taarifa ya pamoja, familia za waathiriwa zimeeleza huzuni kubwa kutokana na vifo hivyo, zikimtaja Adam na Helen kuwa wazazi wenye upendo na waliojitolea kwa familia yao.
Familia hizo zimeeleza kuwa wanandoa hao walikuwa wakijali sana watoto wao, huku maisha yao yakijikita katika kuwalea na kuhakikisha wanapata mazingira yenye upendo na furaha.
Aidha, Anita Maria Cetina ameelezewa kama mlezi aliyekuwa na nafasi muhimu katika familia hiyo, akiwatunza Emma na Charlie kwa upendo, kujitolea na uangalifu mkubwa.
Kwa mujibu wa familia hizo, Anita alikuwa zaidi ya mlezi wa kawaida, akichukuliwa kama sehemu ya familia kutokana na uhusiano wa karibu aliokuwa nao watoto hao.
Familia za waathiriwa zimeomba kuheshimiwa kwa faragha yao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, zikieleza kuwa zinahitaji muda wa kukabiliana na msiba huo mkubwa.
Wakati huo huo, uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea ili kubaini mazingira yaliyopelekea ndege hiyo kuanguka na kusababisha vifo vya watu wote tisa waliokuwa ndani yake.
Mamlaka husika nchini Marekani zinatarajiwa kuendelea kuchunguza sababu za ajali hiyo, ikiwemo hali ya ndege kabla ya kuanguka na mazingira yaliyokuwepo wakati wa tukio.
Vifo hivyo vimeacha familia na marafiki wa waathiriwa katika majonzi makubwa, huku wakiendelea kukumbuka maisha na mchango wa wapendwa wao.
Ajali hiyo ilizua taharuki miongoni mwa jamii haswa wale wanaotumia usafiri wa anga,wakishindwa kujenga imani na baadhi ya makampuni ya uchukuzi wa anga na hivyo kuiomba serikali kuhakiki rubani na chombo chenyewe









