Akiba Ya Kenya Ya Fedha Za Kigeni Yaongezeka, Gharama Za Mikopo Nje Yapungua

Kenya imerekodi ongezeko la akiba yake ya fedha za kigeni huku mapato yanayotolewa na hati fungani za serikali katika masoko ya kimataifa, maarufu kama Eurobonds, yakishuka.

Hatua hiyoainayoashiria mabadiliko katika mazingira ya kifedha ya taifa.
Taarifa hiyo imeangaziwa katika ripoti ya kila wiki ya Benki Kuu ya Kenya (CBK), inayofuatilia mwenendo wa uchumi, soko la fedha na shughuli za kifedha nchini na kimataifa.

Kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni ni muhimu kwa sababu kunaimarisha uwezo wa nchi kukabiliana na mahitaji ya malipo ya kimataifa, ikiwemo uagizaji wa bidhaa kutoka nje pamoja na kulipa madeni ya kigeni.

Akiba hiyo pia hutumika kama kinga dhidi ya misukosuko ya kiuchumi inayoweza kusababishwa na mabadiliko ya bei za bidhaa katika soko la kimataifa, misukosuko ya kisiasa na kuyumba kwa thamani ya sarafu.

Kwa mujibu wa CBK, kiwango cha akiba ya fedha za kigeni hupimwa pia kwa idadi ya miezi ambayo nchi inaweza kuagiza bidhaa kutoka nje bila kutegemea mapato mapya ya fedha za kigeni.

Kwa upande mwingine, kushuka kwa viwango vya mapato ya Eurobonds za Kenya kunaashiria kupungua kwa faida ambayo wawekezaji wanadai ili kuendelea kushikilia hati fungani hizo.

Mabadiliko hayo yanaweza kuashiria kuimarika kwa imani ya wawekezaji katika uwezo wa Kenya kutimiza wajibu wake wa kifedha, ingawa mwenendo huo pia huathiriwa na hali ya masoko ya kimataifa.

Eurobonds ni hati fungani ambazo serikali hukopa fedha kutoka kwa wawekezaji wa kimataifa, huku ikiahidi kulipa riba na kurejesha mtaji kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa.

Hata hivyo, kushuka kwa mapato ya hati hizo hakumaanishi moja kwa moja kuwa deni la taifa limepungua, bali kunaweza kupunguza gharama za kukopa endapo serikali itaingia tena katika soko la kimataifa.

CBK ina jukumu la kusimamia utulivu wa kifedha, kudhibiti sera za fedha na kuhakikisha taifa linakuwa na akiba ya kutosha kukidhi mahitaji yake ya kimataifa.

K