Sasa ni wazi kwamba Winnie Odinga atawania kiti cha Useneta katika gatuzi la Nairobi. Hayo ameyazungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbumbu ya mwaka mmoja tangu baba yake, Raila Amolo Odinga afariki dunia.
Winnie amesema hatua hiyo sio mbwembwe bali ni mpango mkakati ambao tayari ametia nia na lazima ahakikishe kwamba anashika nafasi hiyo kwa manufaa ya watu wa Nairobi na Kenya nzima kwa ujumla wake.
Tangazo lake limeipa Nairobi darubini kuntu ambapo kwamba ambapo kuwa kwa sasa seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anajiandaa kujiondoa katika nafasi hiyo kwani tayari amebuni chama cha Linda Mwananchi, ambacho bila shaka kitamtawaza kuwa mgombea wa kiti cha Urais, mwaka 2027.
Hata hivyo Winnie ametoa tamko hilo akijaribu kukata mnong’ono kutoka kwa watu mbalimbali kwamba amekuwa kimya kwa muda sasa.
Ameongeza kwamba kifo cha baba yhake (Raila), kilichotokea nchini India Oktoba 15,2025 akiwa na umri wa miaka 80, kilimuacha na makvu chungu nzima na hivyo alilazimika kukaa kimya akimuomboleza, hatati mzazi baba yake.
Amesema Sifuna alishinda kiti cha Useneta kwenye gatuzi la Nairobi kupitia chama cha Orange Democratic Movement, (ODM) mwaka 2022 kwenye uchaguzi mkuu na hivyo haoni taabu kupata nafasi hiyo kupitia chama hicho hicho.
Aidha anaelezea kwamba anatamani kuwaona vijana wakimuunga mkono katika kuwania nafasi mbali mbali za uongozi nchini zikiwemo za ugavan, useneta n ahata ubunge.
Ni hapa ambapo Winnie aliwapa changamoto baadhi ya viongozi ambao wamekuwa na kauli zisizoeleweka kwenye nafasi zao huku wengine wakipiga picha na kujisahaulisha, kwa mujibu wa ‘Raila’ alivyokuwa amegawa maarifa.
Hata hivyo, baada ya kifo cha Raila Odinga, kuliibuka mjadala w a ni nani atakayendeleza urithi wa kisiasa.
Aidha, mnamo Oktoba 2026, baadhi ya wazee wa jamii ya waluo walimfanyia Winnie hafla ya kimila iliyomwasilisha kama mrithi wa kisiasa wa baba yake.
Vile vile kutambuliwa kwa Winnie kuwa mrithi wa baba yake hakumpi nafasi ya moja kwa moja kuwa mrithi wa baba yake, licha ya wafuasi wengi kutoka eneo la Nyanza kuwa na matumani makubwa juu yake.









