Washukiwa Saba Wadakwa Limuru
Limuru:Polisi mjini hapa linawashikilia watu saba wanaodaiwa kuwa wahalifu.
Washukiwa hao,inasemekana wamekuwa wakijihusisha na visa vya kihalifu kama vile ubakakaji na wizi wa kimabavu huku wakilenga wananchi na wageni eneo la upanzi wa majani chai na kwingineko likiwemo eneo la Braxton Tunnel.
OCPD wa Limuru,Mary Njoki anasema washukiwa hao wamekamatwa kutokana na ushirikiano wa raia na vyombo vya kiusalama, eneo hilo. Aidha, washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa kwenye mamlaka husika mara baada ya uchunguzi dhidi yao kukamilika.
Afisa Mary anasema wananchi wanatakiwa kuendelea na moyo huo wa kutoa ushirikiano ikiwemo ripoti ili kurahisisha unasaji wa watu wanaodaiwa kuwa wahalifu.
Katika hatua nyingine, polisi katika eneo hilo litaendelea kufanya msako na kuweka doria kabambe ili kuhakikisha kwamba wananchi na mali yao wanakuwa katika hali nzuri ya kiusalama. Mji wa Limuru, upo katika gatuzi la Nakuru na umekuwa ukikumbwa na visa vya kihalifu mara kwa mara.
Kwa njia hii sasa, wananchi watapata afueni ya kufanya shughuli zao zikiwemo za kiuchumi hata masaa ya jioni bila uoga.
Mathlan, suala la ukosefu wa usalama katika baadhi ya ameneno nchini, limetajwa kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo huku asilimia kubwa ya wawekezaji wakisita kutia nia kutokana na wasiwasi wa gharama zao kupotea.
Siku chache zilizopita, Waziri wa usalama nchini Kenya Kipchumba Murkomen, alitaja mikakati kambambe ambayo serikali imenuia kuitumia katika kuhakikisha kwamba mfanyabishara na mwananchi wa kawaida, wanabaki katika mazingira salama, bila kujali hadhi ya mamlaka ya mtu mmoja mmoja.
Hata hivyo, serikali za kaunti na hali kadhalika zile za mitaa zimekuwa zikishirikiana kuhakikisha wananchi wanatoa ripoti kwa vyombo vya dola hususan wakati ambapo mgeni au wageni wameingia kwenye Kijiji au kaya. Hili limesaidia katika kutambua na kuchambua watu, kazi zao na malengo ya yao kuwa eneo fulani kwa nyakati gani. Hata hivyo, vyombo vya sheria kwa kushirikiana na wananchi wenye nia njema, vimekuwa katika msatri wa mbele kuimarisha usalama nchini, licha ya changamoto kadhaa.









