Marinari, wavuvi na watumiaji wengine wa bahari katika pwani ya Kenya wametakiwa kuwa waangalifu zaidi kufuatia utabiri wa hali mbaya ya bahari, ikiwemo mawimbi makubwa na upepo mkali unaoweza kuhatarisha usalama wao.

Tahadhari hiyo inaashiria uwezekano wa hali ya bahari kuzorota katika baadhi ya maeneo ya pwani na maji ya kina kirefu, hali inayoweza kuhatarisha boti ndogo, vyombo vya uvuvi na usafiri mwingine wa majini.

Kwa mujibu wa utabiri huo, upepo unaovuma kutoka mashariki-kusini-mashariki hadi kusini-magharibi-kusini unatarajiwa kuwa na kasi ya kati ya mafundo manne na 24, sawa na takriban mita mbili hadi 12 kwa sekunde.

Hata hivyo, maeneo fulani yanaweza kukumbwa na upepo wenye nguvu zaidi, hali inayoweza kusababisha mawimbi kuongezeka na kufanya shughuli za baharini kuwa hatari.

Hali ya bahari inatarajiwa kutofautiana katika maeneo mbalimbali, huku baadhi yakikumbwa na mawimbi madogo na mengine yakikabiliwa na mawimbi makali hadi makali sana.

Wavuvi wadogo na waendeshaji wa boti wametakiwa kutathmini hali ya hewa kabla ya kuingia baharini na kuepuka safari zinazoweza kuhatarisha maisha yao na wafanyakazi wenzao.

Aidha, waendeshaji wa vyombo vya majini wametakiwa kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa ya baharini na kuchukua tahadhari zinazofaa, hasa katika maeneo yaliyo wazi ambako upepo mkali na mawimbi makubwa yanaweza kujitokeza.

Dhoruba ina uwezo wa kukiangusha chombo cha usafiri baharini ikiwemo boti, feri na hata meli.

Hali hiyo onaweza kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha lakini pia umauti kwa binadamu.

Kufuatia hali hiyo, watu hususan abiria wanatakiwa kupewa darasa kubusiana na kubadilikabadilika kwa mawimbi ya bahari ili kupabga ratiba kamili ya usafiri.

Hata hivyo, madhara ya kimbunga hutokea nara moja baada ya muda mrefu ingawa kinaqeza kusababisha madhara makubwa.

Mara ya mwisho kutokea kwa ajali ya upepo mkali katika Pwani nchini Kenya ilikuwa 2025 ambapo mtumbwi ulizama ukiwa na wavuvi hata licha ya kutolewa kwa tahadhari na mamlaka husika.

Tahadhari hiyo inaashiria uwezekano wa hali ya bahari kuzorota katika baadhi ya maeneo ya pwani na maji ya kina kirefu, hali inayoweza kuhatarisha boti ndogo, vyombo vya uvuvi na usafiri mwingine wa majini.