Kwa muda mrefu sasa, jamii nyingi zimekuwa zikitambulikana kutokana na mila au tamaduni zake.
Tamadauni hizi zinakuwa zinatofautisha jamii au kabila moja hadi jingine.
Kwa mfano,nchini Kenya na Tanzania, jamii ya Kimaasai, ina tamaduni za kuvalia shanga kwenye shingo n ahata kichwani, hususan wakati wa sherehe au maadhimisho
fulani yanaoendana na jamii hiyo.
Shanga hizo, kwa hatua kubwa zinakuwa zimefungwa kwa Pamoja zikiwa na viashiria mbalimbali ambavyo huwa ni siri ambayo mtu wa kawaida au anyetoka jamii nyingine hawezi kuelewa, kirahisi.
Miaka ya elfu mbili na kuendelea, uvaaji wa shanga hususan katika maeneo ya kiunoni, ulinoga.Bidhaa hiyo sasa haikuvaliwa na jamii ya wa maasai tu bali karibia kila jamii barani Afrika, zinavalia shanga.
Katika eneo la Sirari, Wilaya ya Tarime nchiniu Tanzania, The News Booth, imekutana na mmoja katio ya akina mama ambaye wapo maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa mbainti ambao wanabalehe kabla ya ndoa.
Mtaalamu anakuja na jambo
Mogesi Boke 73, ni kungwi, kazi yake ni kutoa elimu hatua kwa hatua kwa mabinti wadogo waliofika kwenye umri wa kubalehe na pia wanawake wanaokabilana na changamoto au migogoro kwenye mahusiano yao.
Kungwi huyu anaeleza kwamba uvaaji wa shanga kiunoni, si jambo jipya bali kitendo cha kuvaa ndicho kinaendelea kuwa kipya, kizazi hadi kizazi.
Anafafanua kwamba, jamii nyingi za barani Afrika, zinavalia shanga za kiunoni, lakini jamii hizo kila moja ina maana yake.Kwa mfano katika mataifa ya Kenya na Tanzania ambayo yanashibana kwenye mambo mengi mbali na Uchumi, anasema uvaaji huyo wa shanga unaaksi vitu kadhaa ikiwemo pambo.
Anaelezea kwamba, uvaaji huu wengine huvalia kama pambo lakini wapo wanaovalia kwa sababu walitakiwa wavae.
Fafanua vema, Kungwi
Anasema, siku hizi idadi kubwa ya wanawake huvalia bidhaa hiyo bila kutambua wala kuwa na sababu ya kimsingi, kama ilivyo katika jamii nyingine.Wapo wanaovaa, madam tu waonekane kwamba wamevalia na wapo wanaovaa kwa sababu maalum.
Kwa mfano, anasema, zipo jamii ambazo zinaaminisha watu wao kwamba, ili kujifungua mtoto wa jinsia fulani, wa kume au kika, ni lazima mwananmke avae shanga kiunoni ndani ya miezi tisa, hadi siku ya kujifungua.
Wakati huo huo anasema wapo wanaovalia kama pambo la kuvutia wanaume au wapenzi wao.
Eleza kwa umakini hapa tuskie
Mogesi, anayetokea jamii ya Wakurya wa Tanzania, anasema kwa sasa dunia imebadilika sana ikilinganishwa na zamani.
Siku hizi watu hususan vijana wamekuwa wakifanya maamuzi bila kujali matokeo yake.
Akirejelea kauli yake ya awali, anasema kuna wanawake wenye Imani kwamba akivalia shanga, atavutia mume au mpenzi wake wakati wakiwa faragha huku pia akiongeza kwamba kuna jamii zilizofunda wanawake namna ya kuchezesha shanga hizo wakati wa tendo.
Anasimulia kwamba, zamani shanga zisingeonekana mchana kweupe kwamba zimevaliwa kiunoni, kinyume na sasa kwamba kuna baadhi ya wanawake huvalia shanga wakati huouo wakiwa na vibode vifupi vya kuruhusu bidhaa au pambo hilo kuonekana hadharani.
Anasema tofauti hiyo ya uvaaji wa shanga kwa vijana umepoteza au kulegeza uhalisia uliokuwepo wa awali ambapo kungwi aliwafundisha wanawake wachanga namna ya kuishi na mwanamume na kabla ya hapo wangeelezewa kipi cha kufanyika ili kummudu mpenzi au mwanaume.
Kauli kutoka kwa wavaaji
Eneo la Mabea, kilometa chache kutoka mjini Migori nchini Kenya, yupo Suguta Matiko 23, ambaye anasema tangu akiwa mtoto mdogo alishuhudiwa mama yake mzazi akiwa anavaa shanga hizo kila ilipotimia mwishoni mwa mwaka, alizibadilisha zote au kufanya mchanganyiko maalum na kuzivalia tgena.
Anasema mama yake, ambaye kwa sasa ni marehemu, aliwahi kumwambia kwamba shanga hizo zilikuwa na maana nyingi ikiwemo maagano ya kitabibu.
Anaelezea kwamba kwa sasa shanga zinatumika kama kivutio kikuu kwa wale wanaopendana huku akihakikishia kwamba ni watu wachache sana watumii pambo hilo.
Aidha anasema katika baadhi ya jamii, uvaaji wa shanga ni sehemu ya hatua moja ya maisha na kuna wakati zinavuliwa ili kuingia hatua nyingine.
Lakini kuna wale wanaosema kwamba shanga za kiunoni zina idadi maalum ambayo kila shanga moja ina taafsriri jambo fulani ambalo mtu kutoka jamii nyingine, kamwe hawezi kuelewa kiulaini.
Hitimisho
Kutoka mijini hadi mashambani, watu wa kike wamekuwa wakishuhudiwa wamevalia bidhaa hiyo kiunoni, b ila kujali yupi wa kuitazama na yapi mazingira ya uvaaji huo.
Mbali na Pwani, shanga huvaliwa tu kama pambo la kuvutia tu na wengi wanakosa maadili wakati wamelivaa kwani hurusu lionekane wakati ambao si sahihi.
Watu wengi haswa wazee wa rika la makamo, wanasema makungwi, wanapaswa kuwa wengi katika kutoa elimu nasaha kwa wanawake wenye ari ya kuvalia shanga, ili kuficha udhlilishwaji wa namna hali ilivyo kwa kizazi kipya.









