Naibu Katibu Mkuu wa Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini (KMPDU), Dk. Dennis Miskellah, ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kikosi Kazi cha Kitaifa kinachoratibu juhudi za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Kenya.
Uteuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Afya Aden Duale kupitia barua ya Oktoba 19, 2026, kufuatia ombi la Katibu Mkuu wa KMPDU, Dkt. Davji Atellah, la kutaka muungano huo ujumuishwe katika timu ya kitaifa inayosimamia mwitikio wa kukabiliana na ugonjwa huo.
Katika ombi lake kwa Waziri Duale, Dk. Atellah alisema ushiriki wa KMPDU ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wataalamu wa afya wanatoa mchango wao wa kitaalamu katika kudhibiti kuenea kwa Ebola.
Alisema kuwa kuhusishwa kwa muungano huo kutasaidia kuimarisha mawasiliano kati ya wahusika mbalimbali, pamoja na kulinda usalama na maslahi ya wahudumu wa afya wanaoshiriki katika shughuli za kukabiliana na mlipuko huo.
Ombi hilo lilifuatia mashauriano yaliyofanywa na Baraza la Kitaifa la Ushauri la KMPDU kuhusu umuhimu wa kuhakikisha kuwa wawakilishi wa wahudumu wa afya wanashirikishwa katika maamuzi yanayohusu usimamizi wa mlipuko huo.
Uteuzi wa Dk. Miskellah unatarajiwa kuipa KMPDU nafasi ya kuwasilisha maoni na mapendekezo ya wataalamu wa afya kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa kudhibiti Ebola, huku ikitilia mkazo usalama wa madaktari na wahudumu wengine walio mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Kikosi kazi hicho cha kitaifa kinasimamia uratibu wa juhudi za kukabiliana na mlipuko wa Ebola, huku ushirikiano kati ya serikali na wataalamu wa afya ukiwa muhimu katika kuimarisha mwitikio wa afya ya umma.
Hizi hivyo hizi ni baadhi ya mbinu ambazo serikali na hata asasi za kiraia zinatotumika katika kuhakikisha kwamba ugongwa wa Ebola unadhibitiwa na hausabai nchini.
Inadaiwa kwamba kufikia sasa taifa la Kenya limeorodhesha zaidi ya kesi saba za maradhi hayo hatari.
Ebola kwa mara ya kwanza iliripotiwa DRC,na baadae maradhi hayo kuanza kusambaa na kuangamiza mamia ya watu wakiome maafisa wa afya kitoka mataifa mbalimbali duniani.









