Staa wa muziki wa Pop kutoka nchini Marekani, Madonna mwenye umri wa miaka 68, amekumbushia tukio la kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza Lourdes Leon, akisema alizaliwa kwa njia ya upasuajin baada ya kuumwa uchungu kwa saa kumi nane.

Mdonna aliyevuma zaidi kupitia nyimbo zake kama La Isla Bonita 1987, na Hang Up 2005, alitoa kauli hiyo wakati akimtakia mwanaye kheri ya kuzaliwa ambapopn ametimiza umri wa miaka 30.

“Kheri ya siku ya kuzaliwa Lourdes wangu, ulinijia katika ndoto. Ndoto yenyehniusia kali.Ndoto inayoitwa maisha.Kama ningejitahidfi kuandika kila kitu, ningelia hadi nikatengeneza mtoto wa machozi,” aliandika Madonna kupitia ukurasa wake wa Instagram
Madonna, mshindi wa Grammy mara saba,alikumb uka changamoto alizokutana nazo wakati wa kujifungua mtoto wake huyop ambaye alizaliwa Oktoba 14, 1996 kwenye hospitali moja mashariki mwa Los Angels, Marekani.

“Baada ya saa 18 za uchungu wa kujifungua, na mapigo yako ya moyo kuanza kupungua, upasuaji wa dharula ili kukutoa tumboni ndio ulikuwa njia pekee ya kukuleta duniani,” aliandika Madonna

Akiambatanisha na picha zao za zamani, Madonna aliongeza kuwa kuzaliwa kwa Lourdes kulikuwa tukio lilovuta sana hisia za watu, huku vyombo vya habari vikifuatilia kwa karibu kilichokuwa kikiendelea hospitalini hapo.

Kuzaliwa kwa Lourdes, ilikuwa furaha kubwa kwa Madonna hadi kuandika wimbo wa Little Star unaopatikana kwenye albamu yake,Ray Of Light, ilioshindwa tuyzo ya grammy ,1998.

Baba mtoto ni Carlos Leon,mkufunzi wa mazoezi ambayo ambaye alikuwa na uhusiano na uhusiano na mwana mama huyo kwenye kipindi hicho.

Kwa sasa, Lourdes ni mwana mitindo aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa, aidha alifanya kazi katika kutanza bidhaa za urembo za mwanamuziki, Rihanna,Savage x Fenty, huku akitokea kwenye kava za majarida makubwa duniani kam vile Vogue na Vanity Fair.

Aidha katika mahusiano mengine na Guy Ritchie alijaliwa kupata mtoto mwingine wa mwisho anayejulikana kama Rocco, aliyeza\liwa agosti 11, 2000 kisha alikuja kuasili (adopt) Watoto wanne kutoka nchini Malawi, ambao ni David, 2006,Mercy 2009 na mapachs Esther na Stella, 2017.