Kirinyaga ina zaidi ya aina 100 za pombe haramu.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kirinyaga, Anderson Njagi, ametoa tahadhari kuhusu kuenea kwa pombe hiyo haramu katika kaunti hiyo.

Amefichua kwamba pombe hizo zenye madhara makubwa, zinapatikana katika eneo hilo.

Njagi amesema Kirinyaga imegeuka kuwa kitovu cha baadhi ya pombe haramu zinazojulikana kwa madhara yake nchini, hali inayozua wasiwasi kuhusu usalama wa wakazi na afya ya umma.

Kauli yake inajiri wakati mamlaka za usalama zikiendelea kukabiliana na biashara ya pombe haramu, ambayo imekuwa changamoto katika maeneo mbalimbali nchini Kenya.

Kamanda huyo amesisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi za kukabiliana na uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa pombe zisizokidhi viwango vinavyohitajika kisheria.

Pombe haramu imehusishwa na hatari mbalimbali za kiafya, hasa pale bidhaa hizo zinapotengenezwa katika mazingira yasiyozingatia usafi na bila kufanyiwa ukaguzi wa kitaalamu.

Baadhi ya pombe hizo zinaweza kuwa na kemikali hatari zinazoweza kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji.

Hata hivyo, idadi kubwa ya bidhaa hizo inazua maswali kuhusu namna zinavyozalishwa, zinavyosambazwa na jinsi zinavyoweza kuwafikia watumiaji licha ya kuwepo kwa sheria zinazodhibiti biashara ya vileo nchini.

Maeneo mengi nchini yamekuwa yakiandaa pombe haramu ambazo ni haramu na hivyo kuhatarisha maisha ya mtumiaji.

Tafsiri yake ni kwamba, waandaaji wa pombe hizo wanadai kwamba wanakosa namna ya kujikimu kimaisha, na hivyo kugeukia biashara haramu ambayo ni kinyume cha sheria.

Karibia kila eneo nchini lina aina yake ya kinywajibau pombe, mfano Kisii wana Chang'aa, Kikuyu Moratina na gongo.

Hata hivyo maafisa wa afya wanasema asilimia kubwa ya watu wanaotumia pombe hizo wapo katika hatari ya kupata maradhi likiwemo la kupofuka macho,kupanuka moyo kutokana na mapigo ya haraka ya moyo na hata kulegea kwa viungo.

Aidha kwenye utafiti, isilimia bwa ya wanywajinpombe hizoni vijana,wanaosema inawalazimu kutumia kinywaji hicho ili kupunguza msongo wa mawazo.

Katika hatua nyingine idara ya usalama imetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kuwafichua waandaaji wa pombe hiyo kwa engo la kutokomeza biashada haramu.