Kampuni ya kusambaza umeme nchini Kenya, Kenya Power, imetangaza kukatizwa kwa huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo ya Nairobi na kaunti ya Meru leo, Ijumaa, Oktoba 16, 2026, kutokana na matengenezo yaliyopangwa kufanywa kwenye miundombinu ya umeme.
Kwa mujibu wa tangazo la kampuni hiyo, huduma ya umeme itakatizwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Katika jiji la Nairobi, maeneo yatakayoathiriwa ni pamoja na Pangani hususan,Forest Road, Chai Road, Agoi Road na Pamba Road, na maeneo jirani.
Katika kaunti ya Meru, hali hiyo itaathiri maeneo ya Mikumbune na Ntemwene, huku wakazi na wafanyabiashara wakitakiwa kujiandaa kwa usumbufu huo wa muda.
Maeneo yaliyotajwa katika tangazo hilo ni pamoja na Mikumbune Market, Gaatia Market, Kandigi C/Fact, Macikine Section, Kiorone, National Oil, Ntemwene, Kagwampungul, Kabyoo na Kieru C/Fact, pamoja na wateja wanaoishi maeneo ya karibu.
Kenya Power imesema matengenezo hayo yanalenga kuwezesha shughuli zilizopangwa kufanywa kwenye mfumo wa usambazaji umeme.
Kukatizwa kwa huduma hiyo kunatarajiwa kuathiri shughuli za kawaida za nyumbani na biashara, hasa zile zinazotegemea umeme kwa ajili ya uzalishaji.
Wafanyabiashara katika maeneo yaliyoorodheshwa wanaweza kukumbwa na changamoto katika utoaji wa huduma, kuhifadhi bidhaa zinazohitaji umeme na kuendesha vifaa vya kielektroniki wakati wa matengenezo hayo.
Kwa sababu hiyo, wateja wamehimizwa kufanya maandalizi mapema ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme.
Kampuni hiyo imewahimiza wakazi kuangalia kwa makini maeneo yaliyotajwa katika tangazo ili kubaini iwapo watakuwa miongoni mwa watakaoathiriwa na zoezi hilo.
Wateja wanaohitaji ufafanuzi zaidi kuhusu kukatika kwa umeme au huduma nyingine wanaweza kutembelea tovuti rasmi ya kampuni hiyo kupitia www.kplc.co.ke au kutumia nambari ya huduma kwa wateja ambayo ni *977#.
Huduma ya umeme inatarajiwa kurejea baada ya kukamilika kwa maboresho yaliyopangwa, ifikapo saa kumi na moja jioni, kulingana na ratiba iliyotangazwa na kampuni hiyo.
Hata hivyo Kenya power kwenye mikakati yake ya kimsingi,kutoa taarifa kwa wateja mapema ni sehemu ya mbinu mahsusi ya kujenga imani kwa wateja wake.









