Mbunge wa Nakuru Mjini (Mashariki),
David Gikaria, anapanga kuelekea Mahakama ya Rufaa kupinga adhabu aliyopewa na Kamati ya Utekelezaji wa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi, huku mawakili wake wakitaka hatua za utekelezaji wa adhabu hiyo zisitishwe hadi rufaa yake iamuliwe.

Katika barua ya Oktoba 16, 2026, kampuni ya mawakili ya Adrian Kamotho Njenga & Co. Advocates imesema Gikaria anakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kamati uliotolewa Julai 14, pamoja na hukumu ya Mahakama Kuu ya Oktoba 8 iliyotupilia mbali ombi lake la mapitio ya kimahakama.

Mawakili hao wamesema watawasilisha ombi la dharura katika Mahakama ya Rufaa wakitaka ulinzi wa muda dhidi ya utekelezaji wa adhabu hizo, wakidai kuwa kuzitekeleza kabla ya rufaa kusikilizwa kunaweza kuhatarisha haki ya mteja wao ya kusikilizwa kwa haki.

Aidha, mawakili hao wanasisitiza kuwa hukumu ya Mahakama Kuu haikumwamuru Gikaria kulipa faini ya shilingi milioni 2.5 wala kutoa ombi la msamaha hadharani.

Wanasema kutupiliwa mbali kwa ombi lake la mapitio ya kimahakama hakumaanishi kuwa mahakama iliamuru adhabu hiyo itekelezwe moja kwa moja.

Wamepinga pia uamuzi wa kamati uliobaini kuwa mbunge huyo alikiuka baadhi ya vifungu vya Kanuni za Maadili ya Uchaguzi ambavyo, kwa mujibu wao, hakuwa ameshtakiwa navyo.

Wanasema suala hilo linazua maswali ya kikatiba kuhusu haki yake ya kusikilizwa.

Katika hatua nyingine,mawakili wanasema kuna baadhi ya vipengele ambavyo kisheria vinapungua kimashikoa hivyo kupunguza maana halisi ya zuio au matakwa ya mteja kama inavyoainishwa kisheria.

Katika hatua nyingine, wachanganuzi wa maswala ya kisiasa nchini wanasema mbunge huyo alipaswa kutoa taarifa mapema,na hili lingesaidia katika kujenga imani kwa wananchi anaowawakilisha na pia kuepuka na sintofahamu ambazo zinaweza kumchafulia jina.

Mathlan,suala la viongozi wa kisiasa kukutwa na figisu za kifedha limekuwa la muda mrefu, huku baadhi wakikutwa wameshiriki moja moja na wengine kuhusishwa bila taarifa zinazoaminika.Badala yake,viongozi wanaishia kumalizia muda wao mwingi mahakamani bafala ya kuwa katika maeneo yao ya uwakilishi na kutatua kero za wananchi wao.